TANZANIA: Chibwa man kufanya kolabo na Christopher Martin, na kuacha kuimba kwa Kiswahili!
29 January 2016

Mkali wa Dancehall Tanzania, Chibwa Man afanya kolabo na Christopher Martin wa Jamaica.
Amesema hiyo ndiyo sababu kwa sasa atakuwa akifanya muziki wake kwa kiingereza zaidi ili kuwafikia watu wengi zaidi.
“Nia yangu nia kubadilisha muziki wa Kitanzania nisiimbe lugha ya Kiswahili kabisa” Chibwa alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM Alhamisi hii.
“Nimeshaanza kufanya track za namna hiyo, nimefanya track na Chris Martin ambayo ni track yangu ya kwanza ambayo nimetumia lugha ya kiingereza. Mimi pamoja na maproducer na timu yangu kwa sasa hawatamani tena niimbe nyimbo kwa Kiswahili, nipo naendelea kufikiria nyumbani ni nyumabni na worldwide ni worldwide tu, kwasababu nataka hela yenye sura ya mtu mwingine sio yule ambaye nimezoea kumuona, kwahiyo niataishika vipi? Inabidi niisongelee kwa jinsi wao wanavyotaka, niisogelee ili iwe karibu nami”, alisisitiza.
Aliongeza “Kwahiyo nipo na timu yangu bado tunajadili zaidi tuendelee kuziokotaokota pesa za Magufuli au tumkimbie tukatafute mbele”.




Leave your comment