TANZANIA: Mwasiti kuachia wimbo mpya na Chidi Benz hivi karibuni
29 January 2016

Mwanadada Mwasiti Almasi anatarajia kuachia wimbo mpya wa ‘Wanipa Raha’ aliomshirikisha Chidi Benz.
Mwanamuziki huyo amekiambia kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM kuwa ingawa rapa huyo ameyumbishwa na mambo ya dunia bado ana nafasi ya kufanya vizuri.
“I wish angerudi kuwa Chidi yule wa zamani ambaye tumemzoea yule wa miaka iliyopita”, alisema Mwasiti.
“Chidi ni mtu mzuri sana labda vitu vilimzunguka wakati ule havikuwa vizuri kwake. Nina ngoma naye kwahiyo watu wataisikia inaitwa “Wanipa Raha”, itatoka soon huu ni mwaka wangu. Nilirekodi naye mwaka jana kwa Mswaki, alikuwa fit na alikuwa anaendesha gari mwenyewe, alikuwa hana matatizo yeyote”.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Mwasiti kufanya kazi na Chidi Benz, miaka kadhaa iliyopita alimshirikisha katika wimbo wake wa ‘Hao’.

Chidi Benz




Leave your comment