TANZANIA: Nahreel toka TZ hadi Nigeria
28 January 2016

Muziki wa Tanzania unazidi kukua kila kukicha, tunashuhudia wasanii mbalimbali wakivuka mipaka na kwenda kimataifa. Kwa sasa pia na maproducer wanajitahidi kutoboa na kwenda mbali, Producer Nahreel wa The Industry ameanza na Patoranking wa Nigeria.
Nahreel ameiambia XXL ya Clouds Fm leo hii kuwa alikutana na Patoranking alipokuja TZ kwenye show, akamsikilizisha kazi kadhaa na kuonekana kupenda kazi hizo, alimtumia beats kadhaa na huenda ujio wa album ya Patoranking ukawa na mkono pia wa kazi ya Nahreel.
Msanii huyo ametayarisha nyimbo kama Don't Bother ya Joh Makini ft AKA, Never Ever ya Vanessa Mdee, Nana ya Diamond ft Mr Flavour na nyingine nyingi.
Kila lakheri kwa Nahreel katika kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.

Patoranking




Leave your comment