TANZANIA: Watayarishaji muziki hatuna umoja - Master Jay

Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Master J amesema siku umoja wa watayarishaji muziki nchini ukiundwa, atarudi rasmi kutayarisha muziki.

Master J ambaye ni mmiliki wa MJ Records, aliliambia gazeti la Mwananchi kuwa, mfumo uliopo kwenye tasnia ndiyo unaochangia kwa kiasi kikubwa kuondoa thamani ya watayarishaji.

“Watayarishaji muziki na waongozaji video wana umuhimu mkubwa katika kukuza muziki hapa nchini, lakini niseme wazi kwamba hatuna maana kutokana na kukosekana kwa umoja baina yetu”, alisema.

“Niliwahi kuitisha kikao kwa lengo la kuunda umoja, ikashindikana. Nimeamua kukaa kando kwa muda ili mambo yakinyooka nirudi upya”

Master J alidai kuwa kutokana na kukosa umoja, kunawafanya watayarishaji wengi wa muziki waonekane hawana maana halia inayowafanya kugawa midundo yao bure.

Leave your comment

Top stories