TANZANIA: Aslay atangaza kuwa single
28 January 2016

Msanii toka kundi la Yamoto Band, Aslay Isihaka atangaza kuwa single. Hapo kabla Aslaya aliwahi kuweka hadharani uhusiano wake na video model aitwaye Tessy Chocolate.
Hata hivyo siku za hivi karibuni muimbaji huyo aliacha kupost picha za mrembo huyo kwenye mtandao wa Instagram kiasi cha watu kuhisi kuwa mambo yameharibika.
Wiki hii Aslay aliiambia E News ya East Africa TV kuwa kwa sasa hana mahusiano nab inti yeyote. Alisema kuhusiana na kinachoendelea katika mahusiano yake, hawezi kukizungumzia kwa sasa mpaka atakapoamua kuweka wazi nini kilitokea. Pia Aslay alishindwa kuzungumzia uvumi uliopo kuwa amemuacha msichana huyo baada ya kupata ujauzito.





Leave your comment