TANZANIA: Mwanamitindo Flaviana azindua bidhaa yake ya rangi za kucha (picha)

Mwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata azindua bidhaa yake ya urembo wa kuccha iitwayo ‘Lavy’.

Akizungumza na waandishi wa habari katika saloon ya ‘Pikasso Beauty Saloon’ iliyopo Posta jijini Dar es salaam, Flaviana alisema anamshukuru Mungu ameweza kutimiza ndoto yake ya muda mrefu.

“Nashukuru Mungu kwakweli hii project nilianza kuishughulikia miaka miwili iliyopita”, alisema Flaviana.

“Kwenye launch ya leo nimelenga kuwaalika watua wenye maduka ya vipodozi na saloon pamoja na marafiki zangu. Kwa maana naamini ukithamini wateja wako hao ndio watakuwa watu wangu wa muhimu. Kwahiyo bidhaa yangu itaingia sokoni kwa bei ya rejareja itakuwa shilingi 5000 na kwa sasa zinapatikana pale Shear Illusions, Picasso na Zuri Cosmetics. Pia kadri tunavyoendelea na jinsi watu wanavyozidi kuomba oda ndivyo zitakavyoenea kila sehemu”.

Mrembo huyo pia alizungumzia suala la ubora wa bidhaa hiyo pamoja na mapango wa kuongeza bidhaa nyngine sokoni.

“Kuna chemical haziruhusiwi kwenye ‘nail polish’. Kila unapotaka kuanzisha product kuna muongozo unapewa. Pia kikubwa zaidi ni ubora wa bidhaa kuweza kukaa kwenye kucha kwa muda mrefu. Hii ni rangi ya kawaida siyo jelly, inakaa siku tano mpaka saba. Kwasababu tayari nilishasambaza kwa marafiki zangu na wamelishuhudia hilo”.

 

Flaviana akiwa na rafiki yake Nancy Sumari

Flaviana akiwa na mtu wake wa karibu

 

Flaviana akiwa na rafiki katika pozi

 

Leave your comment