TANZANIA: Rose Muhando awahishwa hospitali baada ya kung’atwa na nyoka mwenye sumu kali

 

Muimbaji wa nyimbo za injili nchini Rose Muhando alazwa hospitali  tarehe 19 mwezi huu baada ya kung’atwa na nyoka mwenye sumu kali nyumbani kwake Dodoma.

Kutokana na gazeti la Global Publisher, hitmaker huyo wa Nibebe aling’atwa na nyoka mguuni wakati akiingia getini kwake na kukimbizwa hospitali ya Dodoma Area C.

Aliwahishwa hospitali na majirani zake baada tu ya kung’atwa na nyoka.

“Hali ya Rose itazidi kuwa mbaya ana matatizo mengi, anasumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu na sasa hivi tena kang’atwa na nyoka” kilisema chanzo kimoja kama alivyo nukuliwa na gazeti la Global Publisher.

Global Publisher walijaribu kumtafuta Rose kwa kupitia simu lakini simu ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kama Kaka wa mwanamuziki huyo.

“Simu imeachwa hapa nyumbani. Dada yangu amewahishwa hospitali ya Dodoma Area C kwenye kitengo cha dharura baada ya kung’atwa na nyoka mguuni. Aling’atwa na nyoka mkubwa na jeraha alilopata ni kubwa sana”.

Tuhuma za kutoa mimba

Mwaka uliopita mwezi wa 3, 2015 mwanamuziki huyo alikumbwa na skendo ya kutoa mimba. Hata hivyo msanii huyo aliweka wazi kuwa alitoa mimba hiyo kihalali kabisa kutokana na maisha yake kuwa hatarini kiafya.

Ilidaiwa kuwa mimba hiyo ilikuwa ya aibu kutokana na mahusiano batili na mwimbaji injili mwenzake.

Habari hizo zilizua utata mkubwa Afrika Mashariki, hali ya kwamba Tanzania inakataza utoaji wa mimba na adhabu ayke ni miaka saba jela.

Vyombo vya habari vilisema Daktari alimshauri mzazi huyo wa watoto 3 kutoa mimba au kupoteza uhai wake.

“Mimi ni mwanamke mtu mzima na ninaye muogopa Mungu. Siwezi kutoa mimba lakini kuna vitu vingine ambavyo ni vikubwa kuliko sisi wanaadamu” alisema Rose Muhando.

“Mimi ni mama wa watoto 3 na ni mtu mzima, Kwa umri wangu, kwanini nitoe mimba? Nina muonekano wa mtu ambaye hapendi uhai wake?

Nilikuwa nikiumwa gonjwa lisiloeleweka na kusababisha miguu yangu kuvimba kwa miezi mitatu mfululizo, nitawaletea vithibitisho kuwaonyesha kuwa mimi si mtoto wa miaka 18” alisema kwa hasira Rose.

Rose Muhando (miaka 40), ambaye alikuwa mshindi wa tuzo ya Msanii bora wa nyimbo za Injili wa kike mwaka 2008 kwa Afrika, alielezea jinsi alivyosikitishwa na tuhuma hizo kutoka kwenye vyombo vya habari.

Pia alipinga tuhuma za kutaka kufungwa kutokana na kutoa mimba na kuwalaumu maadui zake, watu ambao alifanya nao kazi na baadae kuwaachisha na kujenga chuki dhidi yake.

“Niliamua kuachana na watu wengine katika timu yangu na hiyo imeleta matokeo mabaya, kwa sasa wanajitahidi kuniharibia career yangu kwa hali na mali” alimalizia Rose.

 

 

 

Leave your comment

Top stories