EXCLUSIVE (TANZANIA) – Tunda Man akiri kummis Cassim Mganga ndani ya Tip Top Connection

 

Tunda Man wa Tip Top connection amedai angekuwa na uwezo angemrudisha Cassim Mganga kwakuwa bila yeye kundi hilo halijakamilika.

Mwanamuziki huyo aliyeachia video mpya ya ‘Mama Kijacho’ siku chache zilizopita, amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa Tip Top Connection inakosa mengi kutokana na kuondoka kwa Kassim Mganga.

“Cassim Mganga kiukweli nammis kwasababu hata kwenye nyimbo za Tip Top akiwepo Cassim inakuwa nyimbo imekamilika kwasababu vocal zangu na zake zimepishana kidogo. Unaweza kuona kama Goma la Manzese unatuona tunapanda na kushuka, umuhimu wa Kassim unauona”, alisema Tunda.

“Ni mtu ambaye tunammis kwasababu na yeye sometimes anatumis pia. Lakini pia umuhimu wake tunauona katika nyimbo yaani mtu kama Cassim natamani hata arudi”.

Cassim Mganga, Mb Dog, Keisha pamoja na Z Anto ni kati ya wasanii waliokuwa Tip Top Connection ambapo kwa sasa wanafanya kazi wenyewe.

 

Leave your comment

Top stories