EXCLUSIVE (TANZANIA) – Barakah Da Prince kufanya kolabo na Sauti Sol na Hartband wa Kenya
21 January 2016

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Barakah Da Prince amesema hivi karibuni ataenda Kenya akiwa na producer wa AM records, Bob Manecky kwaajili ya kwenda kufanya kolabo na hitmaker wa ‘Uliza Kiatu’ Hartband pamoja na bendi maarufu Afrika, Sauti Sol.
Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM Jumamosi iliyopita, Barakah amesema lengo lake kubwa la kufanya hivyo ni kubadilisha mziki wake.
Hivi karibuni msanii huyo ameachia video mpya ya ‘Siwezi’, iliyoonozwa na Kevin Bosco Jr. Pia Barakah alitajwa na MTV Base miongoni mwa wasanii 32 wa Afrika wa kuwaangalia mwaka huu.




Leave your comment