EXCLUSIVE (TANZANIA) – Nisha adai alilipwa elfu 50 kwenye filamu yake ya kwanza

Msanii wa filamu na mjasiriamali, Salma Jabu maarufu kama Nisha amesema licha ya sasa hivi kumiliki kampuni yake ya filamu, pesa yake ya kwanza kulipwa katika filamu ilikuwa ni shilingi elfu 50,000.

Mrembo huyo ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wasanii wenye mafanikio kwenye tasnia hiyo ya filamu, amekiambia kipindi cha Uhondo cha E FM kuwa baada ya kuanza kupata mafanikio kidogo kidogo kwenye filamu aliwekeza na kununua vifaa pamoja na kuanzisha kampuni yake.

“Filamu yangu ya kwanza kulipwa nililipwa elfu 50, pesa niliyoitumia kuwekeza hadi leo namiliki kampuni yangu”, alisema Nisha.

Pia Nisha alisema baada ya kupata jina katika filamu na kuanza kupata pesa alijiingiza katika biashara kubwa za nguo ambazo amedai zinamnufaisha zaidi mpaka sasa.

Kwa sasa Nisha anatarajia kauchia filamu mpya ‘Kiboko Kabisa’ iliyotayarishwa chini ya kampuni yake, Nisha’s Film Production.

Leave your comment