EXCLUSIVE (TANZANIA) – Bifu kwenye Bongo Fleva hazina maana – Bill Nas
21 January 2016

Rapper wa ‘Ligi ndogo’, Bill Nas amedai bifu kwenye muziki wa Bongo Fleva ni za kitoto na hazina faida.
Msanii huyo ametoa kauli hiyo wakati akiongea na mtangazaji wa kituo cha Hits FM cha Zanzibar, D’ Only D Swagga kupitia kipindi cha Power Artist.
Bill amedai bifu hizo zinawafanya mashabiki kutoamini muziki wa Bongo Fleva. Na kuongeza kuwa bifu nyingi ni za kawaida ukilinganisha na kati ya marehemu Bito na Castro lililopelekea kifo.
Hivyo amewataka wasanii kuwa kitu kimoja ili kuujenga muziki wa Bongo Flava.




Leave your comment