EXCLUSIVE (TANZANIA) – Ben Pol kufanya kazi na producer mkongwe 'Master J'
21 January 2016

Msanii wa RnB nchini, Ben Pol amesema kuingia studio kufanya kazi na Master J ni heshima kubwa sana kwake.
Hivi karibuni na Izzo Bizness walirekodi wimbo kwa usimamizi wa producer huyo mkongwe wa MJ Records akishirikiaga na Duppy.
“Leo hii upo kwenye project ambayo Master J amekuamini, amekuweka anakusikiliza pale ‘Ben Pol unasemaje una cha kuongeza’, yaani haya ndo maisha yangu naishi kwenye ndoto yangu. Ni feeling fulani ambayo ni nzito kidogo”, Ben alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM kilichozinduliwa tena rasmi Jumamosi iliyopita.
Tazama kipindi hicho hapa;
Ben Pol amesema mwaka huu anatarajia kufanya video mbili ambapo moja itakuwa ya nyumbani na yenye uswahili mwingi lakini itakayokuwa na picha za kuvutia. Ya pili amesema itakuwa zile anazodai watu wamezizoea zenye magari ya kifahari na wasichana warembo.




Leave your comment