EXCLUSIVE (TANZANIA) – Kundi la Mapacha kuja na kipindi cha Televisheni “50/50”

 

Rappers wa kundi la Mapacha wanatarajia kuja na kipindi cha TV kiitwacho ‘50/50’ kitakachozungumzia maisha yao na marafiki zao.

Akizungumza na 255 ya XXL ya Clouds Fm Jumanne hii, mmoja kati ya Mapacha hao amesema kipindi hicho kitaanza kuonekana hivi karibuni.

“Ni kipindi cha ‘50/50 TV show’ kinakuja hivi karibuni kwahiyo nafikiri watu wakae tayari kukisubiria lakini pia ni kipindi ambacho kinahusu maisha yetu na marafiki zetu na watu wnaotuzunguka”, alisema.

Ameongeza kuwa umewachukua muda mrefu kukiweka sawa kutokana na mambo yote kuyafanya kwa fedha zao wenyewe.

“Tunashukuru Mungu tunazidia kuvuka vikwazo na vikwazo ni vingi kama unavyojua sisi hatujapata sponsor wa kusimamia kipindi hiki kwahiyo ni hela ambazo zinatoka mifukoni mwetu ndio maana kimechukua muda mrefu kukamilika”.

Lakini pia hawajaweka wazi ni Televisheni ipi kipindi chao kitakua kikionyeshwa.

Leave your comment

Top stories