EXCLUSIVE (TANZANIA) – Nilianza kuitwa baba tangu nikiwa kidato cha pili – Nay Wa Mitego

Msanii wa Bongo Fleva, Nay Wa Mitego alianza kuitwa baba akiwa kidato cha pili.

Mambo hayo yalitokea baada ya kumzalisha msichana wa kihindi aliyefukuzwa kwao na kuwalazimu kutafuta chumba cha kupanga na kuishi pamoja wakati Nay akiendelea kusoma sekondari.

Ambapo hiyo pia ilitokea miaka michache baada ya kuwa amefukuzwa kwao akiwa darasa la saba na kwenda kuishi salon.

“Nilipofika form two nilikutana na mwanamke wa kihindi ambaye ndiye nimezaa naye mtoto wa kwanza aliyekuwa ananisaidia ada”, amesema Nay kwenye kipindi cha Chill na Sky.

Nay anasema baada ya girlfriend wake kufukuzwa kwao walienda kutafuta nyumba ya kupanga Manzese lakini walishindwa kupata chumba kwakuwa walionekana wadogo sana kiumri.

Anasema walibidi waende kutafuta chumba maeneo ya Kimara ambako walifanikiwa. Nay anasema girlfriend wake alimsaidia fedha ya ada pamoja na hela ya kwanza kwenda kurekodi wimbo wake kwa P-Funk.

Sikiliza kipindi kizima cha Chill na Sky hapa chini;

Leave your comment

Top stories