EXCLUSIVE (TANZANIA) – Nilificha mambo mengi mabaya kulinda penzi letu na Shilole – Nuh Mziwanda
18 January 2016

Nuh Mziwanda amedai aliyofanyiwa na Shilole ni mengi na mazito ambayo ilibidi ayafiche kwa maslahi ya penzi lao na heshima yao.
Akiongea kwenye kipindi cha D’Weekend Chat Show cha Clouds Tv ijumaa iliyopita mbele ya Shilole aliyekuwa amejikunyata pembeni kwa kukasirishwa na uwepo wa ex wake studioni hapo bila kutaarifiwa mwanzoni, Nuh alisema Shilole hakuwa mwanamke wa kutawaliwa.
“Yeye anajua mambo gani alikuwa anafanya kwangu, mambo ambayo alikuwa hastahili anifanyie. Alikua anafanya kwa kunichukulia poa kwamba nitafanya nini lakini at the end of the day kila kitu kina mwanzo na mwisho” alisema.
Nuh alisema ni ngumu kurudisha moyo wako kwa mpenzi wako huyo licha ya kukiri kuwa bado hajaweza kuwa tayari na mwanamke mwingine kwa sasa.




Leave your comment