EXCLUSIVE (TANZANIA) – TCRA kufungia vituo 22 kwa muda wa miezi 3 zikiwemo Star Tv, RFA, Kiss FM, Radio 5 na Radio Uhuru!

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Ally Simba

 

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imevifungia vituo 21 vya redio na sita vya runinga kwa kipindi cha miezi 3.

Adhabu hiyo imetokana na vituo hivyo kushindwa kulipia ada ya leseni, iliyoanza rasmi jumatatu ya tarehe 18 januari.

Vituo vya Sahara Media Group ndivyo vilivyoathirika zaidi. Vituo vya redio, Radio Free Africa na Kiss FM pamoja na kituo cha runinga Star Tv vilivyo chini ya kampuni hiyo vyote vimefungiwa.

TCRA imedai kufikia hatua hiyo baada ya vituo hivyo kukiuka sheria ya Utangazaji ya Posta ya Mwaka 2014 ambayo imevitaka vituo hivyo kulipia ada ya leseni ya matangazo kwa kila mwaka na ada ya masafa.

“Kifungu cha 22 cha sheria ya EPOKA ambayo ipo sura ya 306 kifungu cha 21(g) inasema kuwa kampuni inaposhindwa kulipia ada ya leseni inapewa siku 30 ili aweze kulipa lakini hawa tumewapa taarifa lakini wamekaidi na wengine wanadaiwa tangu mwaka jana, kwahiyo sheria inasema wazi na sisi tumewapa notice ya siku 30 na bado wakawa wanasuasua kulipa, tumevifungia kwa miezi mitatu”, Afisa Habari wa mamlaka hiyo, Innocent Mungi aliiambia blog ya Full Habari.

Vituo hivyo vilivyoanza kuzima matangazo usiku wa jumapili jan 17, lakini habari njema ni kwamba kwa wale watakaolipa deni hilo ndani ya muda huo wataruhusiwa kurudi hewani.

“Katika kipindi cha miezi 3 kituo chochote kikilipa deni ada ya leseni na kutimiza matakwa yote ya kisheria na pesa zote anazodaiwa basi sisi tutamfungulia”, alisema Mungi na kusisitiza kuwa kama kituo kitashindwa kulipa ada hiyo ndani ya kipindi hicho na kitanyang’anywa kabisa leseni.

Hii ni list ya vituo vilivyofungiwa;

  • Sibuka FM
  • Country FM
  • Breezy FM
  • Ebony FM
  • Hot FM
  • Impact FM
  • Iringa Municipal TV
  • Kiss FM
  • Radio Free Africa
  • Kitulo FM
  • Kifimbo FM
  • Mbeya City Municipal FM
  • Radio 5
  • Musa Television Network
  • Pride FM
  • Radio Huruma
  • Radio Uhuru
  • Star TV
  • Rock FM Radio
  • Standard FM
  • Sumbawanga Municipal TV
  • Tanga City TV
  • Top Radio FM Limited
  • Ulanga FM

 

Leave your comment

Top stories