EXCLUSIVE (TANZANIA) – Unataka kujua kwanini Joh Makini hapendwi kufananishwa na rapa wengine? Hii ndiyo sababu..

 

Rapper Joh Makini anayehit na kibao cha ‘Don’t Bother’ amesema mashabiki na watu wanaopenda kuwafaninisha rappers, ndio wanaosababisha kuwepo na ugomvi usiojenga tasnia ya muziki.

Akizungumza na 255 ya XXL ya Clouds FM Alhamisi hii, Joh amesema hali hiyo inawafanya wasanii wengine wajisikie wapo chini na kusababisha chuki.

“Sipendi kwasababu tangu naanza muziki wangu kuna njia zangu ambazo napita. Sio kitu kibaya watu kufananisha kwasababu si wote tunafanya Hiphop” alisema.

“Lakini wakati mwingine hivi vitu vinazua chuki, watu wengine hutengeneza picha ambazo ni tofauti. Kama wewe mwenyewe ni shahidi sisi kama Weusi hatujawahi kumuongelea msanii yeyote vibaya na kutengeneza chuki. Tunajaribu sana kukwepa hivi vitu kwasababu tulishagundua hivi vitu havijengi kwenye industry bali vinabomoa. Sisi tunalenga zaidi kwenye kujenga na kuendeleza kuibrand Hip Hop ya Tanzania kwenda kwenye level nyingine za kibiashara”, aliongeza.

“Mimi ukiniambia mambo ya conscious ama sio conscious siyajui. Mimi nafanya muziki kutokana na feeling yangu na ninavyoandika muziki wangu nakuwa conscious”.

Leave your comment

Top stories