EXCLUSIVE (TANZANIA) – Beka Ibrozama aachia video ya cover ya Hello (Adele)

 

Wasanii mbalimbali wamefanya cover ya wimbo wa Hello yakwako Adele iliyopo katika album yake ya 25 iliyotoka novemba 20 mwaka jana, na hii hapa ni kutoka kwake msanii Beka Ibrozama.

Msanii (Beka) huyo ameamua kufanya cover ya wimbo huo ili kuonyesha mashabiki duniani uwezo wake wa kuimba.

“Ni wimbo fulani mgumu sana, ni wimbo wenye sauti za juu, una melody nzuri na ili uweze kupita kwenye hizo njia ni lazima kidogo uwe unajua muziki” anasema Beka.

Msanii huyo alijipatia umaarufu mkubwa kwa wimbo wake wa ‘Natumaini Remix’ aliouandika kwa ufundi mkubwa huku akitumia kuunganisha mantiki ya wimbo huo kwa kutumia majina na nyimbo mbalimbali ya wasanii.

Tazama hapa cover hiyo ya Hello;

Leave your comment