EXCLUSIVE (TANZANIA) – Mandojo na Domokaya waja na Studio mpya

 

Wasanii wa muziki, Mandojo na Domokaya wamefungua studio mpya mbali na uwekezaji wanaoufanya katika biashara zao mbalimbali. Wameamua kufungua studio kwa lengo la kuwasaidia wasanii wengine kufikia mafanikio kimuziki.

Akizungumza katika kipindi cha E News cha East Africa Television, Mandojo alisema studio yao tayari imeshaanza kufanya kazi.

“Sisi kwa sasa hivi studio tumeshaifungua ipo kinondoni. Domokaya ndiyo yupo pale anasimamia kwasababu tunakuwa na producer tofauti tofauti yaani hata kama msanii ana producer wake anaweza akaja nae”, alisema Mandojo.

“Pia tayari kuna wasanii ambao tupo nao ndani ya label na tukiona kuna wasanii wengine  wana uwezo tunawasaini. Sasa hivi tunataka kufanya muziki wa kitofauti kidogo kwasababu mwanzoni tulishafanya harakati za muziki. Kwahiyo sasa tunataka tuwekeze nguvu zetu kwenye huu muziki wa bongo fleva hasahasa kusaidia vijana wapya ambao hawajapata nafasi”, aliongeza Mandojo.

Mandojo na Domokaya waliwahi kutamba na nyimbo kama Nikupe nini, Wanoknok na nyingine.

 

Leave your comment