EXCLUSIVE (TANZANIA) – Rapper G Nako apoteza Tsh. Milioni 6 kwenye kikao cha wasanii (Audio)
8 January 2016

Rapa kutoka kundi la Weusi, G Nako amepoteza kiasi cha dola 3,000 kwenye kikao cha wasanii kilichofanyika tarehe 5, januari 2015, maeneo ya Little Theather karibu na Protea Hotel.
Katika You Heard ya SoudyBrown wa Clouds FM ya tarehe 6, januari ametoa taarifa hiyo kuwa G Nako amepoteza kiasi hicho cha fedha alipokuwa kwenye kikao cha wasanii.
Alipatikana Baba Levo, ambaye amesimulia kwamba mazingira yanaonyesha G Nako alikaa sehemu ambayo alizungukwa na watu wake wa karibu ambao sioa rahisi kumwibia, hivyo huenda pesa hiyo kaangusha.
Nikki wa Pili ambaye ni msemaji wa Weusi amesema bado hawajajua ni mazingira yapi pesa hizo zimepotea lakini zilikuwa ni dola 3,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 6.5.
Pole kwa msanii G Nako kwa kupoteza kiasi hicho cha fedha.
Sikiliza hapa audio ya taarifa hiyo;




Leave your comment