EXCLUSIVE (TANZANIA) – Je, unamjua msanii wa Tanzania aliyetajwa kutazamwa zaidi 2016 na mtangazaji wa BBC Radio 1Xtra ya Uingereza!
5 January 2016

Mwaka unapoisha wafuatiliaji mbalimbali wa muziki huwa kwenye nafasi nzuri ya kuwafanyia tathmini wasanii kutokana na kazi walizofanya mwaka mzima, ambapo hutoa miongozo ya kutabiri nafasi ambazo wasanii hao wanaweza kuwa nazo kwa mwaka unaofata.
Mtangazaji wa BBC Radio 1Xtra ya Uingereza, DJ Edu ametaja orodha ya wasanii wake watano wa kuwatazama zaidi mwaka 2016, kutokana na kufanya vizuri mwaka 2015. Katika orodha hiyo amemtaja muimbaji wa Tanzania, Vanessa Mdee aka ‘Vee Money’ ambaye amemuweka kwenye nafasi ya 2. Wengine aliowataja ni 5. A Pass (Uganda), 4. Runtown (Nigeria), 3. Donald (Afrika Kusini) na 1. Ston Bway (Ghana).

Vanessa Mdee
DJ Edu hutangaza katika kipindi cha chati ya muziki, DNA Top 5 ambayo hujumuisha kazi za muziki za wasanii mbalimbali wa Afrika ikiwemo Tanzania.

DJ Edu.




Leave your comment