EXCLUSIVE (TANZANIA) – DJ wa Jay Z kuburudisha siku ya mwaka mpya jijini Dar (Video)
30 December 2015

Dj wa Rapa Jay z, anayeitwa DJ Young Guru anayefanya kazi za udj katika show zake, ametua kwa mara ya pili nchini Tanzania.
Young Guru amesema anajisikia vizuri sana kwasababu tayari alipata marafiki kadhaa alipotua kwa mara ya kwanza na alifahamiana pia na baadhi ya watu, hivyo mara hii si mgeni kabisa.
Pia jambo lingine linalompa furaha ni kuwa ndani ya Tanzania akiburudisha mashabiki mbalimbali kwenye usiku wa Grown and Sexy December, 31, 2015 wakati wa mkesha wa party ya kuupokea mwaka mpya wa 2016.

AY (kushoto) na Young Guru (Kulia)
Pia Young Guru anawakumbuka baadhi ya marafiki zake akiwemo AY, Mwana FA.
Tazama hapa interview yake na Millard Ayo akiwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam;




Leave your comment