EXCLUSIVE (TANZANIA) – Adam wa Visual Lab kuwaunga mkono wanaoenda kushoot video nje!

 

Muongozaji wa video nchini Adam Juma wa Visual Lab amesema sio kitu kibaya kwa wasanii kwenda kushoot video zao nje ya nchi ikiwa kuna faida yoyote ya ziada wanayoipata.

Adam ambaye amekuwepo katika soko la muziki kwa muda mrefu, amesema kuwa kikubwa anachoamini kinachowapeleka nje wasanii ni kutafuta connection na mawazo mapya na hilo sio jambo baya.

“I think ubora hatuko tofauti sana lakini pia labda ni mawazo mapya, siwezi kusema kwamba ubora uko tofauti, ndio wana vifaa vizuri lakini hata sisi tunavyo, mwisho wa siku it doesn,t really matter wache waende nje wakashoot, kama director najiamini na nina mawazo, na kama itawasaidia kwenye biashara yake kuongeza pesa hiko ni kitu kizuri”, alisema Adam Juma kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.

Pia ameongeza kuwa hadi sasa ameshindwa kuelewa ni kwanini video zinazotayarishwa na waongozaji wa hapa nyumbani hazipati nafasi kwenye vituo vikubwa vya nje licha ya kuwa na ubora sawa na zile zinazofanywa na madirector wengine.

“Siwezi kusema ni upendeleo na inawezakana ni upendeleo, kwasababu kuna kazi unaweza ukatuma mtu anakwambia sija download intaneti bei ghali, lakini sio kama ubora uko tofauti hapana, lakini hata sisi kuna madirector wanafanya vizuri”, aliongeza Adam.

Ambapo suala hili la maswali mengi limeibuka baada ya siku chache zilizopita msanii Afande Sele kuwadis wasanii wanaenda kushoot nje kuwa ni usaliti wa nchi.

Leave your comment

Top stories