EXCLUSIVE (TANZANIA) – Bila Fella kimuziki mimi si kitu –Chege
28 December 2015

Rapper Chege amesema anaamimi yeye pamoja na Mheshimiwa Temba bila boss wao hawawezi kufanya kazi ya muziki bila kumtegemea, Saidi Fella.
Msanii Chege ambaye ameachia wimbo mpya wa ‘Sweety Sweety’ hivi karibuni aliowashirikisha Runtown, na Uhuru, amekiambia kipindi cha FNL cha EATV kuwa boss wao huyo amekuwa akisimamia kila kitu kwenye muziki wao.
“Sisi bado tupo chini ya mkubwa Fella na kufanya kazi bila yeye tunaona tutayumba na kupotea” alisema Chege.
“Mimi mpaka leo sijui gharama ya video yangu mpya, kazi yote kafanya Mkubwa, mimi natumwa tu nenda kule. Kwahiyo Fella kwenye muziki wetu ndiyo kila kitu”, aliongeza Chege.
Waakati katika hatua nyingine, Fella amewshukuru mashabiki wake kwa kuufanya wimbo huo kuwa mkubwa




Leave your comment