EXCLUSIVE (TANZANIA) – Baby J asema sababu inayofanya wasanii wakike kushindwa kutoka

 

Msanii wa muziki, Baby J amezitaja sababu za wasanii wengi wakike kushindwa kufikia malengo yao kimuziki.

Mwanadada huyo ambaye yupo chini ya uongozi wa Mkubwa na Wanawe wa Saidi Fella, amesema kuwa moja kati ya sababu kubwa inayowafelisha wasanii wakike ni mfumo wa muziki wa zamani ambao ulitawaliwa na wanaume wengi.

“Kuna kitu ambacho mimi sasa hivi sitaki kukiangalia, nilikuwa nikiangalia zamani kwenye muziki.Watu wanawasaidia wasanii ni wanaume pekee, hakuna meneja mwanamke wala producer mwanamke, wala hakuna director wa muziki mwanamke”, amesema Baby J.

“Kwahiyo hiyo hali ilitufanya tuwe wakusaidiwa kila siku. Pia tunakutana na changamoto ya kuwekewa vikwazo kutokana na kuwakataa au wale unaokubali kudeal nao wanaanza dharau na kukuchukulia poa. Lakini sasa hivi tunashukuru Mungu wasanii wakike wamepata njia na mwanga kama mimi, tunamuona Vanessa yupo katika level ya juu na mimi inanifanya nijivunie uwepo wake, pia inanifanya niongeze bidii kuwa kama yeye”, alisema Baby Jay.

Pia mrembo huyo amewataka mashabiki kusubiri kazi nyingi mpya ambazo zimesimamiwa na management yake mpya.

Source: Bongo5

Leave your comment

Top stories