EXCLUSIVE (TANZANIA) – Ben Pol aeleza sababu ya Avril kutokuonekana kwenye video ya Ningefanyaje

 

 

Hivi karibuni msanii Ben Pol ameachia video ya wimbo wa “Ningefanyaje” aliowashirikisha Anvril na Rossie M, lakini matarajio ya wengi ilikuwa kuwaona wote walioshirikishwa katika wimbo huo.

Lakini ilikua tofauti, ambapo Ben Pol ametoa sababu ya mrembo Anvril kutokuonekana katika video hiyo ambayo kwake ameitaja kuwa kubwa kuliko zote alizowahi kuzifanya.

Video hiyo iliyoongozwa na Justin Campos wa Afrika Kusini, Ben Pol ameonekana akiimba na Rossie M ambaye pia ameshirikishwa kwenye wimbo huo huku mashabiki wakiisikia sauti ya Anvril bila kumuona mwimbaji huyo.

Katika taarifa rasmi aliyoitoa kwenye vyombo vya habari, Ben Pol amewaomba radhi mashabiki wake kwa kuwapa video ambayo haijakamilisha wahusika wote hususani kutokuonekana kwa Anvril, na kusema kwamba sababu zilizopelekea hivyo zilikua nje ya uwezo wa pande zote katika utayarishaji wa video hiyo.

 

 

Pia Ben Pol amesema pamoja na kuwa na maandalizi makubwa, video ya ‘Ningefanyaje’ ilikumbwa na changamoto nyingi tangu awali zilizopelekea kuahirishwa mara tatu.

“Kwa kweli hii video tokea mwanzo ilikuwa na changamoto, kwanza tulisogeza mbele karibia mara tatu tena tukiwa tayari tumefika Afrika Kusini mimi na Rossie” alisema Ben Pol. “Mara ya kwanza ni kutokana na ‘delay’ ya Viza upande wa Anvril. Si unajua Wakenya wao wanaenda South kwa Viza tofauti na sisi Tanzania hatuendi kwa viza so kwetu ni rahisi zaidi muda wowote tu ukiamua fasta unaenda”, aliongeza.

Mkali huyo wa RnB alieleza kuwa baada ya tarehe mpya kupangwa na muongozaji aliyeshoot video hiyo, Justin Campos, siku moja kabla ya kushoot, ANVRIL alipata tatizo lingine ambalo lilimzuia kusafiri kwa siku iliyofata kwenda Afrika Kusini.

Wakati huo huo Campos naye alimueleza Ben Pol kuwa kwa jinsi ya ratiba yake ilivyo endapo ataahirisha tena kushoot video hiyo, ratiba yake isingemruhusu hadi Januari au Februari 2016, kitu ambacho Ben Pol hakutaka kutokana na kwenda tofauti na ratiba zake.

“Kutokana na hali hiyo, sikuwa na jinsi nyingine zaidi ya kukubali matokeo ya kwasababu mwisho wa siku si mimi wala Anvril wala director aliyekwamisha bali ni ‘situation’ ambayo ilikuwa nje ya uwezo wa kibinadamu”, aliongeza Ben Pol.

Itazame hapa video ya Ningefanyaje.

Leave your comment

Top stories