EXCLUSIVE (TANZANIA) – Hiki ndicho alichokijibu Alikiba baada ya Ben Pol kumwandikia Post Twitter!!
23 December 2015

Wiki iliyopita msanii Ben Pol aliandika ujumbe ulioleta utata akimuuliza msanii Ali Kiba kuhusu jambo fulani, lakini mashabiki wakachukulia kitofauti.
Ben Pol alidai kuwa alikuwa akitaka kumtumia kitu kile alichoandika private lakini akakuta bahati mbaya amepost sehemu ya wazi na kila mtu akaona.
Ali Kiba kwa upande wake ameyasema haya wakati akihojiwa na Soudy Brown wa Clouds FM kwenye kipindi cha U-Heard, alisema yeye amechukulia poa post ya Ben Pol kwasababu yeye ni muungwana na anamtanguliza Mungu mbele.
“Najiona nina mchango mkubwa kwenye BongoFleva na ni mmoja wa malegendary wakubwa ambao bado tupo kwenye muziki.. Ben Pol sio rafiki ni msanii mwenzangu na tunaheshimiana ..tuko vizuri sina mambo ya kuweka vitu rohoni”, alijibu AliKiba.
Tweet hiyo ilisomeka hivi;
"Bro @OfficialAliKiba mi naona kama unakua overrated halafu Halafu inakugharimu..au Haikugharimu".




Leave your comment