EXCLUSIVE (TANZANIA) – Kushoot video nje ya nchi ni usaliti – Afande Sele

 

Msanii mkongwe nchini Afande Sele amedai kuwa anawashangaa wasanii wanaoenda kushoot video zao nje ya nchi, wakati Tanzania ina kila kitu.

Rapa huyo mkongwe aliyekuwa kimya kwa muda kutokana na shughuli za kampeni, amesema kuwa anaamini wasanii wanaosafiri kwaajili ya kushoot video nje ya nchi, wana biashara zao za siri na ni usaliti.

“Kwenda kushoot video nje ya nchi ni ulimbukeni” alisema Afande Sele.

“Tanzania tuna kila kitu kuliko hata huko wanakoenda, Mimi hii naitafsiri kama usaliti wa nchi, sisi tunakosa nini hapa nyumbani? Tuna milima, mbuga, maporomoko mazuri, yaani tuna kila kitu. Unajua wasanii wengi walikuwa wanatumia mwanya wa kwenda kushoot video nje ili kufanya biashara zao za siri. Wengi wametumia sana huu mwanya, sasa Magufuli alivyoingia atawanyoosha tu”, aliongea Rapa huyo.

Pia Afande Sele ameongeza kuwa anajipanga kuachia nyimbo mpya mbili kufidia ukimya mkubwa aliouacha kwa mashabiki wake.

Source: Bongo 5

Leave your comment

Top stories