EXCLUSIVE (TANZANIA) – Kuna umuhimu kwa msanii kutoa album – Mwana FA

 

Msanii wa muda mrefu katika muziki wa Bongo Fleva na anayefanya vizuri hadi hivi sasa, Mwana FA ambaye kwa sasa anafanya muziki wake katika level za kimataifa ametoa msimamo wake kwa msanii kuhusu utoaji wa album.

Mwanamuziki huyo ameachia nyimbo ya ‘Asanteni Kwa Kuja’ hivi karibuni, wimbo huo ambao video yake imefanyika nchini Afrika Kusini, ameeleza hayo katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio.

“Kufanyika album ni lazima laini tuje na idea ni jinsi gani tutauza, tunaweza kufanya hii kazi ya distribution wenyewe, au tunaweza kuwafikia wale watu ambao wahindi hawawafikii, ninachofikiri si tumekwama hatukuwa na investment kwenye muzikia au hatujafungua vichwa vyetu”, alisema FA.

Pia Mwanafalsafa amegusia suala la tofauti ya nuziki wa sasa na ilivyokuwa enzi za ‘Ingekuwa Vipi’.

“Si tulianza muziki kipindi ambacho hatukuwa tunaamini kwamba muziki utatuingizia hata elfu kumi, sasa hivi hatuna wasanii wengi wa kutoa album wanahesabika”, aliongezea Mwana FA.

Leave your comment