EXCLUSIVE (TANZANIA) – Dully ndiye Godfather katika muziki wangu - Mabeste
22 December 2015

Msanii wa muziki aina ya Rap, Mabeste ameweka wazi jinsi msanii mkongwe Dully Sykes alivyomsaidia katika wakati mgumu maishani mwake.
Mabeste ambaye kwa sasa yupo katika mapumziko ya sikukuu za mwisho wa mwaka katika mbuga za Manyara National Park, Arusha. Ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa Dully ndiye Godfather katika muziki wake.
Msanii huyo amesema kwa kipindi chote alipokuwa akihangaika na muziki, Dully Sykes ndiye alikuwa msaada kwake, kuanzia kuvaa, kula na kulala na aliishi nyumbani kwa Dully kwa muda mrefu.
Katika hatua nyingine Mabeste amekanusha taarifa zinzozagaa kuwa amepotea baada ya kuachana na label ya B’ Hits.
“Niliondoka B’Hits nikiwa nimepanga chumba kimoja hata TV sina, lakini nilipoanza kufanya kazi zangu mwenyewe nikahama mbagala na kuhamia Kinondoni nikapanga upande mzima wa nyumba, nikanunua gari na maisha yakaendelea kama kawaida, kwahiyo kimuziki nilishuka lakini sikuyumba kimaisha” alisema Mabeste.




Leave your comment