EXCLUSIVE (TANZANIA) – Lollipop ajishindia tuzo ya “Wimbo wa Mwaka” kwenye Xtreem Awards za Kenya
21 December 2015

Mtayarishaji, mtunzi na muandaaji wa muziki, Goodluck Gozbert maarufu kama Lollipop amefanikiwa kuanza kuona mafanikio ya kipaji chake kwa kushinda tuzo ya kwanza, Xtreem Awards 2015 zilizotolewa Nairobi, Kenya Jumapili Dec, 20.
Ambapo Gozbert ameshinda katika kipengele cha ‘Tanzania Artist/Song of the Year’ ambapo alikuwa akishindana na waimbaji wengine wa muziki wa Injili wakiwemo Bony Mwaitege, Edson Mwasabwite, Enock Jonas, Christopher Mwahangila na wengine.
Mtayarishaji huyo wa Hit Song za Barakah Da Prince “Siachani Nawe” na “Nivumilie”, pamoja na “Basi Nenda” ya Mo Musi na kueleza tuzo aliyoshinda ina maana gani kwake.
“Hii tuzo imefanyika hatua kubwa sana kwenye muziki wangu, motisha kwa malengo yangu lakini pia imefanyika kuwa kumbukumbu katika maisha ya muziki wangu kwa ujumla hasa ukizingatia ndio tuzo ya kwanza kabisa kwangu lakini pia tuzo toka nje ya mipaka ya Tanzania. Nimefarijika sana, na kwangu moja ya hatua kubwa ambayo sitosahau na kuiheshimu", alisema Lollipop.
Na pia alitoa shukrani kwa Watanzania waliompigia kura na kumpa ushindi huo.
“Napenda kuwashukuru Watanzania wote na mashabiki wa muziki wangu nje na ndani ya Tanzania kwa kunipigia kura lakini pia vyombo vyote vya habari, wadau wa muziki mbalimbali na watu binafsi waliojitolea kwa namna moja au nyingine kunifikisha hatua hii, nawashukuru sana”, alimaliza msanii Lollipop.

Muwakilishi wa Goodluck akimpokelea tuzo yake Kenya.
Source: Bongo 5




Leave your comment