EXCLUSIVE (TANZANIA) – Berry Black aeleza sababu ya kuvunjuka kwa kundi lao!

 

Msanii Berry Black aliyekuwa anaunda kundi la Berry Black & Berry huko nyuma, na inawezekana umekuwa ukitamani kujua sababu ya kuvunjika kwa kundi hilo.

Pia msanii huyo amehamisha makazi yake kutoka Zanzibar na kuhamia jijini Dar es salaam huku kazi zake zikiwa zinasimamiwa na Mkurugenzi wa TMK Wanaume Family, Said Fella.

Msanii huyo ametoa sababu ya kundi lao kutengana kupitia MillardAyo.com na kusema “Chanzo cha kuvunjika kundi letu ni kutokana na kutoelewana ndipo nikaamua niwe natoanyimbo zangu peke zangu siunajua ustaa ukishakua staa tena kwahiyo 2006 likavunjika, mwisho wake tabia zikabadilika kati yangu na Berry White” alisema Berry Black.

Pia aliongeza kuwa “ Sisi tulikuwa hatuna kiongozi tofauti na makundi mengine tulikuwa tupo tu na ndio chanzo cha kuvunjika kwa kundi.. kwa sasa makazi yangu nimeyahamishia Dar es salaam na kazi zangu zinasimamiwa na Mkubwa Fella”.

Source: MillarAyo.com 

Leave your comment

Top stories