EXCLUSIVE (TANZANIA) – Video mpya za MB Dog zimemgharimu zaidi ya million 90!

 

 

Msanii wa muziki aliyetamba kwa kipindi cha nyuma, MB Dog, amesema tayari ameshakamilisha maandalizi ya video za nyimbo zake mbili alizozifanya nchini Afrika Kusini ambazo zimemgharibu $45,000 ambazo ni zaidi ya milioni 90 ya Kitanzania.

Muimbaji huyo anayesimamiwa na kampuni ya QS J Mhonda, amesema mpaka sasa hivi tayari video moja ya wimbo wa ‘Sio Siri’ ameshakabidhiwa.

“Jumla ya video zote ni dola 45,000 tumefanya video mbili moja ipo tayari na moja naenda kuimalizia after one week. Na hiyo pesa tumeilipa tu hiyo kampuni, yaani tukisema nikae nipige hesabu yote kwa ujumla ni pesa nyingi sana”, amesema MB Dog.

Pia MB Dog amesema kupitia kazi hizo ana  imani zitamrudisha katika kazi yake hadhi yake.

“Video moja ya wimbo ‘Sio Siri’ itatoka hivi karibuni na nina imani hii kazi itakuwa nzuri na mashabiki wataipokea. Kwaiyo mimi nawaomba mashabiki wangu pamoja na wadau wa muziki waoneshe ushirikiano ili kupeleka mbele muziki wetu”.

Amesema video hizo zimeongozwa na muongozaji wa Afrika Kusini akishirikiana na Aby Kazi.

Source:Bongo 5

Leave your comment

Top stories