EXCLUSIVE (TANZANIA) – Lord Eyes apania mwaka wa 2016

 

 

Rapper kutoka kundi la Weusi ameonesha kuupania mwaka 2016, kwa kuufanya mwaka wa kulipa madeni anayodaiwa na mashabiki wake waliomkosa kwa muda mrefu.

Ukimya wake ulioleta maswali mengi ikiwemo la kama ametengana na Weusi ulivunjwa baada ya Rapper huyo hivi karibuni alipoweka wazi kuwa bado yupo Weusi.

“Napenda kuwaambia mashabiki zangu kuwa mwaka 2016 ni mwaka wangu sasa kufanya kweli, kwani ukimya wangu umeendana na kupika kazi na mpaka sasa nimeshafanya kazi mbili na G Nako vitu vinakuja kwenye masikio yao wakae mkao wa kula”, alisema Lord Eyes kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.

Hapo awali Weusi walimsimamisha Rapa huyo kutokana na matatizo yaliyojitokeza miezi kadhaa nyuma ya rapa huyo kuhusishwa na wizi na baadaye walimsamehe.

Leave your comment

Top stories