NEW SONG(TANZANIA) – Raisi Magufuli Kutungiwa wimbo na Kalapina "Magufuli Balaa"

 

Aliyekua mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni kupitia Chama cha Act Wazalendo na Mwanamuziki wa Hip Hop Kalapina ameamua kuandika wimbo na kuingia studio unaomhusu Raisi Magufuli. Wimbo huo unaitwa ‘Magufuli Balaa’ , umetengenezwa na Dunga kwenye studio za 41 Records.

Hii imetokana na baada ya Raisi Magufuli tangu apate wadhifa huo ameendelea kukonga nyoyo za watu na mataifa mbalimbali kutokana na ufanyaji wake kazi. Pia katika kuadhimisha siku ya Uhuru jana 9 Disemba, alitoa ari na nguvu kubwa ambayo imehamasisha Watanzania wengi kufanya usafi katika mazingira mbalimbali kama alivyoamuru.

Sikiliza hapa;

 

Leave your comment

Top stories