EXCLUSIVE (TANZANIA) – Thamani ya muziki wangu itapanda zaidi nikifa – Q- Chief

 

 

 

Msanii Q-Chief anayetamba na kibao cha ‘For You’, amesema kuwa hata akifa leo muziki wake utapanda thamani maradufu kutokana na nyimbo zake kuwa nzuri.

Mwanamuziki huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, kuwa uwezo wake wa kutunga nyimbo za kuishi muda mrefu utawafanya wanae waishi maisha mazuri baadaye.

“Mimi sikupiga muziki ambao ni bubble gum, mimi nimepiga muziki unaoishi kuliko maisha yangu. Nikifa leo value yangu inakuwa mara tatu ya mimi kuwa hai, and therefore unaweza hata kuwasomesha watoto wangu, na kuwaendeshea maisha yao kwasababu wengi wananifuata kutaka kupiga remix ya ngoma zangu, lakini naangalia anaenda kuiwaste au anaenda kuitengeneza?” alisema.

Pia hivi karibuni Q-Chief aliachia wimbo ‘Mkungu wa Ndizi’ akiwa na TID.

Leave your comment