EXCLUSIVE (TANZANIA) – Mashabiki mtatukosanisha wasanii kwa kutushindanisha – Vanessa Mdee
8 December 2015

Mwanadada Vanessa Mdee anayetamba na kibao cha ‘Never Ever’ kwa sasa, amewataka mashabiki waache tabia ya kuwashindanisha wasanii au kuwagandamiza ili mmoja wao aonekane yupo juu.
Akizungumza kupitia kipindi cha Planet Bonga cha EATV jana, Vanessa alisema kila msanii ana nafasi yake katika muziki, ndio maana ni vigumu kuwalinganisha.
“Kuna baadhi ya mashabiki sio wote, wenye tabia ya kugandamiza wasanii. Tabia ya kupambanisha wasanii kwasababu wana kitu fulani au ambao wanafanya kitu similar hii siyo hali nzuri”, alisema Vanessa.
Na kuongeza, “Game ni ngumu kama mnavyoona, sasa tukianza kujadiliana sijui fulani ni fulani tunaweka ugumu kwenye lengo letu la kutengeneza muziki mzuri na kuleta burudani. Kwahiyo mimi nampenda Shaa. Shaa ni mwanamke ambaye amekuwa kwenye game kwa miaka 10, amefanya kazi kubwa sana”.
Kauli hiyo ya Vanessa ameitoa baada ya Shaa kuulizwa anajisikiaje pale ambapo msahabiki wanapompambanisha na Vanessa.
“Niwaambie ukweli sipendi kabisa hii tabia ya watanzania kunishindanisha na Vanessa Mdee au kitendo cha kuwashindanisha wasanii wa nyumbani” Shaa aliiambia Planet Bongo ya EATV.




Leave your comment