EXCLUSIVE (TANZANIA) – Kala Jeremiah kutambulisha wimbo wa “Malkia” ijumaa hii
7 December 2015

Rapper Kala Jerimiah kutambulisha wimbo na video ya “Malkia” Ijumaa hii ya tarehe 11/12/2015. Ambapo ni kwa muda mrefu mashabiki wake wamekua wakisubiri ujio wa wimbo huo alioahidi angetoa kabla ya mwaka 2015 kuisha.
Katika uzinduzi wa wimbo huo Kala Jeremiah atasindikizwa na Roma, Izzo Bizness, Malaika na Dayna Nyange.
Ambapo video ya wimbo huo imeongozwa na director Pablo ambaye pia alifanya nae video zake zilizopita. Kupitia ukurasa wake wa instagram Kala Jerimia amewataarifu mashabiki zake kuhusu utambulisho huo kwa kuandika,
"iJUMAA HII TAREHE 11-12-2015 NAZINDUA WIMBO MPYA WA #MALKIA NA VIDEO YAKE PALE CLUB BILZ KWA KIINGILIO CHA TSH 10,00. NIAMINI MIMI UKIFIKA HAUTAJUTIA. KARIBU UIONE KWA MARA YA KWANZA @malkia_wa_karne".
Tazama baadhi ya picha za video hizo hapa;






Leave your comment