EXCLUSIVE (TANZANIA) – “Burger Movie Selfie” Kutambulishwa wiki ijayo kwenye Trace Urban
4 December 2015

Tunapoelekea kufunga mwaka huu wa 2015 Belle 9 amefanikiwa kupiga hatua nyingine katika muziki wake, ambapo wiki ijayo video ya wimbo wake wa ‘Burger Movie Selfie’ itaanza kuonyeshwa kwa mara ya kwanza na Trace Urban.
Ambapo hii itakuwa ni video yake ya pili ya Belle 9 kwa mwaka huu na toka ameanza muziki kupitishwa na kuoneshwa na chaneli hiyo ya kimataifa baada ya wimbo wake wa ‘Shauri Zao’ ambayo inapewa airtime ya kutosha.
Kitu kizuri kuhusu video hii, Belle 9 ni mtu wa Morogoro, video imeshutiwa na Morogoro na muongozaji wa video aitwaye GQ ambaye ni wa Morogoro , na mtayarishaji wa audio Tiddy Hotter wa Morogoro japo alikuwa akifanya kazi Mwanza na sasa amehamia Dar es salaam.
Ambapo Trace ilipost katika ukurasa wao wa Twitter na kuandika;
What's up Trace Family! Watch "Burger Movie Selfie" by @bellenine starting next week on @TRACE_Urban channel #325 on @DStv_Kenya




Leave your comment