EXCLUSIVE (TANZANIA) – Huwa sisikilizi nyimbo zangu – Ben Pol

 

 

Mkali wa R&B Bongo Ben Pol amesema huwa hasikilizi nyimbo zake licha ya kuandika nyimbo nzuri na kuwapa mashabiki burudani.

Ben Pol ameyasema hayo alipohojiwa katika kipindi cha XXL cha Cloud Fm, amesema huwa hasikilizi kabisa nyimbo zake anazokuwa ameachia tayari.

“ Nahisi nikisikiliza nyimbo zangu ambazo zimeshaenda redioni kuna uwezekano wa kurudia kuandika kitu ambacho nimeshakitoa ndiyo sababu kuu huwa sipendi kusikiliza nyimbo nilizoachia radio” alisema Ben Pol.

Leave your comment