EXCLUSIVE (TANZANIA) – Kaa tayari kwa video mpya toka kwa Chege Jumatatu ijayo
3 December 2015

Msanii Chege baada ya kukaa kwa muda wa wiki 3 nchini Afrika Kusini,sasa arejea nyumbani Jumatano hii.
Jumatatu ya wiki ijayo Chege ataitambulisha video ya wimbo wake aliomshirikisha msanii wa Nigeria Runtown.Chege amesema akiwa nchini humo pia alikutana na wahusika wa TV mbalimbali kubwa za Afrika ili kutambulisha kazi yake mpya na kupewa ratiba ya uzinduzi.
“Nilikuwa kwenye mazungumzo ya kupewa ratiba ya kuachia video kwenye TV kubwa na nashukuru Mungu nimerudi jana na leo nitapewa ratiba kwa ajili ya TV za nje, kwahiyo kikubwa ilikuwa connection”, alisema Chege.
“Viongozi wangu walishafanya kazi hiyo na mimi ilikuwa ni kumalizia tu. Pia ratiba kidogo nimebadilisha, ngoma ilikuwa itoke kesho tarehe 4, ila tumeahirisha na tumepanga itoke tarehe 7, video ndio ianze kutambulisha. Kwahiyo mashabiki wasubiri kazi nzuri”, amesema Chege.
Source: Bongo 5




Leave your comment