EXCLUSIVE (TANZANIA) – Ijumaa hii Baghdad kuachia wimbo mpya wenye sauti 70 za watu mashuhuri
3 December 2015

Wasanii wengi wanaachia nyimbo zao kipindi hichi cha kufunga mwaka, nae Rapper Baghdad ni kati ya wasanii hao ambapo anategemea kuachia wimbo mpya kesho Ijumaa.
Bagdad anasema wimbo huo utavunja rekodi kwa kuwa na sauti 70 za watu maarufu.
Wimbo huo unaitwa ‘Unaakili Wewe?’ akiwa amemshirikisha Roma.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Baghdad ameandika
“Wimbo mpya wa Baghdad na Roma unatoka tarehe….4th December ijumaa!! Wimbo huo umevunja rekodi, kwakuwa wimbo uliohusisha watu maarufu/mashuhuri zaidi ya 50! Ndani ya wimbo huo utawasikia watu maarufu 70 wakiwemo viongozi wa serikali na dini, wasanii wa bongo flava na bongo muvi, wanasoka, wanamitindo, watangazaji, djz, producers! Na nafasi walizoshiriki katika wimbo huo!!! Unaakiliwewe?”.




Leave your comment