EVENT (TANZANIA) – Roberto wa Amarula kutumbuiza Dar Disemba 11
3 December 2015

Hitmaker wa wimbo wa “Amarula” kutoka nchini Zambia anatarajia kutumbuiza jijini Dar es salaam. Msanii huyo atatumbuiza pale viwanja vya Escape 1, Mikocheni.
Ambapo hii ni mara ya kwanza kwa msanii huyo wa Brotherhood Music Crew kutumbuiza Dar ila ya pili kwa Tanzania kwakuwa miezi kadhaa iliyopita alitumbuiza jijini Mwanza.
Baada ya Dar Roberto aliyeletwa na kampuni ya C&G Solutions ikishirikiana na Freconic Ideaz atatumbuiza pia jijini Dodoma kwenye Instagram Party.
Hivi karibuni Roberto aliachia remix ya Amarula akimshirikisha Patoranking wa Nigeria. Pia anafanya kazi na Mavin Music na Reekado Banks.
Tazama video ya Amarula hapa;
<iframe width="560" height="315" src="https://www.youtube.com/embed/ZBloeWs7N1I" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>




Leave your comment