EXCLUSIVE (TANZANIA) – Nahreel kusikitishwa na kitendo cha kutotambulishwa katika wimbo wa Nana
3 December 2015

Baadhi ya watu hawafahamu kuwa wimbo wa 'Nana' umeandaliwa na Producer Nahreel wa The Industry, na hii ni kwasababu haina ule utambulisho wa kazi zake ‘Nahreel on the Beat’ ambao husikika katika kazi zote alizotayarisha.
Nahreel amesema kiashirio cha producer kwenye wimbo kimeondolewa kwasababu ambazo hakuona kama zina uzito.
“Sababu walizosema walisema tu stori ilivyoanza pale mbele ile slogan yangu ingeleta hitilafu lakini it doesn’t make sense, kwahiyo ndo walitoa hiyo sababu, lakini mimi niliona it doesn’t make sense hata kama hiyo slogan ingekuwepo isingeharibu chochote” Nahreel alisema kupitia Planet Bongo ya EA Radio.
Kutokana na kitendo hicho Nahreel amewashauri watayarishaji wengine kuwasainisha wasanii mikataba itakayowabana wafate makubaliano ya kazi ikiwemo kutoondoa utambulisho wa mtayarishaji kwenye beat.
“Kwanza sisi maproducer wenyewe tuwe strong kwenye hili suala, tukazie msanii anapokuja studio hizo slogan lazima kuweka hata na mkataba fulani kwamba hii slogan lazima iwepo, ukitoa hii kazi is no longer yours. Kuwe na kitu fulani ambacho kitaweza kumbana msanii, na kwahiyo tuanze kuwabana wasanii hapa studio na kukubaliana kabisa”, aliongeza Nahreel.
Tazama video hiyo hapa;
<iframe width="560" height="315" src="https://www.youtube.com/embed/IflpfcHmq5I" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>




Leave your comment