EXCLUSIVE (TANZANIA) – Christian Bella kuachia kolabo yake na Koffi Olomide kabla hajatua Bongo

 

 

Mwanamuziki mkongwe toka DRC Kongo anatarajia kuja Tanzania kutumbuiza wiki ijayo, hivyo hiyo imemfanya Christian Bella kuamua kuitoa kolabo waliyoifanya pamoja kabla hajafika nchini.

Bella amesema wimbo tayari umekamilika na amepanga kuutoa mapema kabla Koffi hajaja ili aweze kutumbuiza naye wimbo huo ambayo ni kolabo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wake.

“Ninajipanga wiki hii au next week ndio nitaachia, kwasababu Koffi anakuja Tanzania ndio sababu itabidi niachie. Anakuja kufanya show yaani naweza kuperform nae inabidi niachie audio” alisema Christian Bella.

Bella ameongeza kuwa pia mpango wa video ya wimbo huo unaendelea na utafanyika hivi karibuni.

Source:Bongo5

           

Leave your comment