EXCLUSIVE (TANZANIA) – Mwana FA kuja tena na hii “Asanteni kwa kuja”

 

 

Mwana FA anakuja tena na single inayoitwa “Asanteni kwa Kuja”. Single hiyo zimeandaliwa na Hermy B na Pancho.

Mwana FA na Hermy B wakikutana huwa wanafanya mambo makubwa na single zao huwa zinahit. Unazikumbuka single kama ‘Habari ndiyo Hiyo’, ‘Bado Nipo Nipo’, ‘Naongea Na Wewe’, ‘Msiache Kuongea’, ‘Naona Nazeeka Sasa’ na ‘Nangoja Ageuke’?

Hizi zote zilipigwa na Hermy B kwenye studio za B’Hits na sasa wanakuletea ‘Asanteni Kwa Kuja’.

FA ambaye alikaa kimya kwa kipindi tangu alipoachia ‘Kiboko Yangu’ akiwa na Ali Kiba, kwa sasa anavunja ukimya kwa kukuletea ngoma hiyo ambayo ina kila dalili za kuwa ngoma kali.

Hermy B ameungana na Pancho kutengeneza ngoma hiyo. Kaa tayari kuipokea.

Leave your comment