EXCLUSIVE (TANZANIA) – Kwanini Diamond huwa hashiki simu ya Zari? Soma sababu hapa

Diamond Platnumz ameweka wazi sababu ya yeye kutoshika simu ya mpenzi wake Zari, na kusema kuwa huwa hawapendi kupekuliana simu zao ili kuepukana matatizo yanayotokana na simu za mikononi.

Simu huleta matatizo na mifarakano katika mahusiano kutokana na meseji au picha za watu wengine na kusababisha ugomvi kati ya wapenzi.

Zari na Diamond ni watu maarufu na wenye mashabiki wa jinsia tofauti, hivyo wameamua kuaminiana na kutambua mazingira ya kazi zao kwa kutokupekuliana simu zao.

“Hicho ni kitu cha kwanza ambacho siwezi kudiriki kabisa”, alijibu Diamond alipoulizwa na Millard Ayo kama huwa anashika simu ya Zari.

Pia Diamond aliongeza kuwa yeye huwa hapendi kushika simu ya mpenzi wake kwasababu ni maarufu pia na anafahamiana na watu wengi hivyo hataki kuumia moyo.

Na alipoulizwa kama Zari pia hushika yake alijibu hivi “Simu yangu mimi haina password naiachaga tu lakini nafikiri nayeye ni mtu wa dizaini hizo ambaye hataki kabisa kudiriki kushika simu yangu, yaani simu zinaleta ugombanishi sana”, aliongeza Diamond.

Pia Diamond aliwashauri watu wengine kutokushika simu za wapenzi wao ili kuepukana na matatizo yanayowezekana kuepukika.

“Kwahiyo simshauri mtu kushika simu ya mpenzi wake, cha muhimu tu kuzingatia kama anakupenda na anakujali na anakuheshimu umuone hivyo tu. Lakini kwenye simu yake umuache afanye chochote anachojua yeye”. Alimaliza Diamond.

 

 

Leave your comment