EXCLUSIVE (TANZANIA) – Vaileth iliingiza shilingi milioni 150- Matonya
27 November 2015

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Seif Shaaban maarufu kama 'Matonya', ameuelezea wimbo wake wa kitambo wa ‘Vaileth’ kuwa ndio wimbo uliompatia pesa nyingi na kwa haraka.
Akizungumza katika kipindi cha The Jump Off cha Times FM, Matonya alisema wiki kadhaa baada ya kuachia ngoma hiyo, alijikuta akiwa na pesa nyingi kwenye account yake.
“Vaileth was a crazy song kwakweli”, alisema Matonya, “Ulikuwa wimbo mkubwa sana, nlipokea simu nyingi kutoka Marekani na kwingineko, yaan ulipagawisha watu kiukweli. Sasa sikuwahi kushika hela nyingi kweli yaani, pesa zangu nyingi zinaingia benk tu, sasa ile siku natazama akaunti naona kama milioni 150 afu haraka tu” alisema Matonya.




Leave your comment