EXCLUSIVE (TANZANIA) – Kumbukumbu ya miaka mitatu tangu Sharo Millionea afariki

 

 

Leo Novemba 26, 2015 ni siku ya kumbukumbu ya Sharo Milionea ambae ametimiza miaka mitatu tangu alipofarikia kwa ajali ya gari.

Sharo alipata ajali na gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T478 BVR alilokuwa akiendesha kutoka Dar es salaam kuelekea kijijini kwao Lusanga wilaya ya Muheza, Tanga.

Muda sio mrefu ambapo msanii na mwigizaji marehemu Sharo Milionea ametimiza miaka mitatu toka afariki, mmoja wa rafiki zake ambae ni mchekeshaji na mwigizaji Kitale ameweka picha Instagram na kuandika “Leo ni tarehe 26/11/2015 na marehemu alifariki 26/11/2012 tarehe kama ya leo ni Miaka 3 sasa tokea Afariki Marehemu Hussein Ramadhani Mkiety kwa ajali ya gari Mkoani “TANGA” Eneo la “MAGUZONI” wilaya ya “MUHEZA” msiba ulikuwa kijijini kwao LUSANGA Na tulimzika kijijini kwao hapohapo LUSANGA anapoishi mama yake mzazi R.I.P Sharo Milionea……….Naomba Tumuenzi Kwa Pamoja Leo ndugu yetu MBELE YAKE NYUMA YETU"– mkudesimbaoriginal

Leave your comment