EXCLUSIVE (TANZANIA) – C9 kuingia mkataba na Panamusiq

 

 

 

Kampuni ya kusimamia wasanii wa muziki Panamusiq wanayofuraha kuwajulisha kuwa Producer mkubwa Tanzania Charles Francis ( C9 ), ameingia mkataba wa muda mrefu pamoja na kampuni hiyo kwa Dar es salaam.

Charles Francis ni mtoto wa mwisho katika familia ya kitanzania yenye watoto 9 (jina la kisanii C9) na mtayarishaji anayeheshimika kwa kazi zake nzuri, kama Mbona Silali (Rich Mavoko), Amerudi (Christian Bella/ Malaika Band), Suna (Barnaba), Mtima Wange (Amini ft Linah) na Dudu (Shilole ft Q. Chillah).

Alianza kuendeleza fani yake ya uprodyuza kwa kufanya kazi na Chuchu FM ya Zanzibar ambapo alikuwa akitengeneza matangazo. Na baadaye alifanya kazi na KIRI records na kisha kuamua kuanzisha studio yake mwenyewe inayoitwa C9 Rekodz.

Kipaji cha C9 kilitambulika pale alipochaguliwa kuwania tuzo za Tanzania Kilimanjaro Music Awards katika kipengele cha ProducerBora wa Mwaka 2013/2014.

Katika mkataba huo Panamusiq wamesema kuwa kutakuwa na muunganiko mkubwa katika kutengeneza na kutoa miziki ya kiafrika yenye viwango bora. Wasanii wengine ambao wapo chini ya Panamusiq ni Linah, Feza na Kioo ambaye ni msanii mpya atayetoa nyimbo zake mapema mwakani 2016.

Taarifa zaidi katika kusign na wasanii zitatoka hivi karibuni.  

Source: Panamusiq press release.

Leave your comment